Header Ads

;

Fella kuwatambulisha warembo 6 wapya kwenye muziki | Joh Music TV

Meneja wa Yamoto Band, Mkubwa Fella amejipanga kulitambulisha kundi jipya la wasanii 6 wa kike baada ya kuona kuna uhaba wa wasanii wa kike katika game la muziki wa Tanzania.
Akizungumza na Joh Music TV Jumatatu hii, Fella amesema tayari ameshafanya maandalizi, na sasa yupo kwenye hatua za mwisho za kupendekeza jina la kundi hilo. “Unajua muziki bongo una wasanii wengi wakiume kuliko wakike, lakini nataka kujaribu kuchangamsha game, nitawatambulisha wasanii wapya sita,” alisema Fella. “Bado hatujawapa jina, lakini tupo kwenye maandalizi ya mwisho, kwa hiyo soon utasikia wakitambulishwa pamoja na project zao,” aliongeza. Katika hatua nyingine, Fella amesema katika kuhakikisha jiji la Dar es salaam linakuwa safi, kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli pamoja na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, kundi lake la muziki, Yamoto Band pamoja na Mkubwa na Wanae, limeachia wimbo mpya ‘Dar ya Makonda’ ambao una hamasisha watu kufanya usafi.

No comments