Header Ads

;

Mafikizolo waeleza wimbo wao na Diamond ‘Colors of Africa’ unamaanisha nini

Zimesalia siku tano tu ile collabo inayosubiriwa kwa hamu Afrika katika ya Mafikizolo na Diamond iachiwe. Video yake itaoneshwa kwa mara ya kwanza Ijumaa hii kwenye kituo cha runinga cha MTV Base. Member wa kiume wa kundi hilo, Theo ameeleza maana ya wimbo wao unaotafsiriwa kwa Kiswahili kama ‘Rangi za Afrika.’ “Colors of Africa ni wimbo unaohusu kusherehekea sisi tulivyo kama watu wa waafrika na unahimiza umoja na kufanya kazi pamoja,” ameandika Theo kwenye Instagram. “Watu wa Afrika ni watu wanaovutia, wazuri na wakarimu. Tuna upeo na wenye vipawa, tumebarikiwa kuwa na bara zuri lenye madini mengi, tunahitaji kujielemisha wenyewe, kujiinua wenyewe na ujuzi na elimu kufurahia faida za utajiri wa bara letu,”ameongeza. “Tunahitaji kujiinua wenyewe kwa kufanya kazi pamoja – biashara, muziki, mitindo, elimu, michezo, afya nk.” Wimbo huo umetayarishwa na DJ Maphorisa wa kundi la Uhuru aliyeshirikishwa pia. Jiunge na Joh Musictz sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za Master ! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Joh Musictz!

No comments