Header Ads

;

Mess Chengula f/ Upendo Nkone – Moyo Wangu Hauna Woga [Official VIDEO]

Miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na mapinduzi makubwa si tu katika muziki wa Bongo Flava, bali pia kwenye muziki wa injili nchini Tanzania.
https://youtu.be/_kV8ZRZkeDw
WATCH/VIDEO
Baadhi ya waimbaji wa sasa wa muziki huo wanatumia gharama kubwa zaidi kutengeneza video za nyimbo zao ili kuhakikisha kuwa zinakuwa na viwango vya kimataifa. Miongoni mwao ni Mess Chengula ambaye ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Moyo Wangu Hauna Woga’ aliomshirikisha muimbaji nguli wa gospel nchini, Upendo Nkone.
Wimbo huo unapatikana kwenye album yake mpya yenye jina hilo hilo ‘Moyo Wangu Hauna Woga’ itakayokuwa na jumla ya nyimbo nyimbo nane. “Nategemea kutoa album tarehe 15 mwezi 6 katika mfumo wa audio na video nyimbo zote zimeshutiwa kwa kiwango cha kimataifa,” Mess ameiambia Bongo5. Mess amesema lengo lake ni kutengeneza muziki wa injili wenye kiwango cha kimataifa na ambazo kiwango cha video zake hakitofautishwi na zile za wasanii wa Bongo Flava. Itazame video hiyo kali hapo juu. Unaweza kuupata wimbo huo hapa hapa Joh Musictz.

No comments