Header Ads

;

New | Kadjanito - (one more night) MP3 Audio Download

https://my.notjustok.com/track/download/id/93370
Jina langu ni Khadija Said Maige. Nilizaliwa Feb 4 kule Kisesa , Mwanza, wazazi wangu wakahamia Tabora na kule nikaanza shule ya msingi katika shule ya Nyasa 1, tukahamia Dar es Salaam na kujiunga na shule ya Kibasila na kumaliza shule ya msingi. Nikajiunga na elimu ya sekondari katika shule ya Actas Mbezi. Wakati wote huu nilianza sana kupenda kuimba na hata nyumbani wakawa wananisifu kuwa na weza jambo ambalo lilinifanya nijaribu bahati yangu kwenye lile shindano la Bongo Star Search, niliondolewa mapema, nikaambiwa sijui kuimba. Mwaka 2008 nilisikia habari ya Tanzania House of Talent, THT, nikaenda ili nijiunge katika uimbaji. Niipofika kule nikakuta watu wanaimba vizuri sana nikabadilisha msimamo kabla hata ya kuanza kusailiwa na nikajieleza kuwa mimi nimekuja pale kujua taaluma ya dancing. Nilikaa kwa muda mfupi maana roho ilikuwa ikiuma kuwaona wenza ngu wakiimba na mimi nikawa mcheza show, fani ambayo sikuipenda sana. Nilikuja kurudi tena THT 2011 , safari hii nikafanya interview nikapasi na kuanza mafunzo rasmi ya kuimba. Baada ya hapo nikarekodi wimbo wangu wa kwanza MAUMIVU katika studio za hapo THT na video ikatengenezwa na Legendary Music. Na sasa nimetoa wimbo wangu wa pili Nzogo ambao maana yake ni NJoo kwa Kisukuma, video pia iko tayari.

No comments