Header Ads

;

Baada ya Shilole kumsaini ‘Gaucho’ kwenye label yake, atangaza habari njema kwa wasanii wa kike

Baada ya hivi karibuni msanii Zuwena Mohammed ‘Shilole’ kupitia label yake ya ‘Shilole Entertainment’ kumsaini msanii Amaselly ‘Gaucho’, ameanza mchakato wa kuongeza msanii wa kike katika label hiyo.
Shilole na msanii wake mpya aitwae Amaselly
Muimbaji huyo wa wimbo ‘SayMyName’, amesema kupitia mafanikio aliyoyapata kwenye muziki anaweza kuwasaidia wenzake.
“Wanasemaga kutoa ni moyo sio utajiri, mpaka hapa nilipo kuna watu walionisaidia na kunifikisha hapa nilipo ndio maana leo naitwa Shishi baby na nyuma yangu kuna wengi wanaonitegemea. Moyo wa shukran ni mzuri ukisaidiwa japo wengi hawanaga shukrani wala hawakumbuki walipotoka. Hivyo na mimi ninajiona mwenye jukumu la kuwasaidia wengine wengi ambao wanahitaji sapoti yangu. Kumsaidia mtu sio lazima uwe na uwezo mkubwa, Gaucho amepata bahati chini ya ‘Shilole Entertainment’ kuwa msanii wa kwanza kabisa kumtambulisha kwenye lebo ya kibabe kabisa, acha na mimi nijilipue tu,” aliandika Shilole kipitia instagram.
Aliongeza, “Huu ni mwanzo tu, nimeanza na huyu anamtafuta mdada anaeweza, mkali na yupo tayari kupambana tupige kazi, kuna mengi yanakuja Mungu atusimamie inshaAllah,”

No comments